Posted in Flagyl on September 17, 2015

Na, Gordon Kalulunga.

WAKATI mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli, akiwa anazungumzia kuwa atahakikisha anadhibiti wizi wa dawa katika hospitali za serikali, wafanyabiashara wameendelea kupandisha bei za dawa katika maduka binafsi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili mkoani hapa, umebaini kuwepo mfumuko wa bei kwa dawa mbalimbali za binadamu pamoja ba huduma za afya hasa ya mother na mtoto.

Bei ya kapsuli moja ya Amoxycilline yenye 250 mg ambayo bei ya jumla ni Shilingi 30, katika maduka ya dawa ya watu binafsi inauzwa zaidi ya tsh 100 na zaidi sawa na asilimia 333. 

Kidonge kimoja cha Metronidazole chenye 200 mg ambacho kwa bei ya jumla ni shilingi 10, lakini wastani wa bei ya duka la madawa ni tsh 50, sawa na asilimia 500.

Aidha uchunguzi zaidi umebaini kuwa, mbali na bei za dawa hizo, pia kuna biashara zingine zinafanyika katika maduka hayo ya dawa muhimu.

Katika suala la huduma za mother na mtoto hususani sindano ya kizuia mimba iitwayo DEPO, hospitalini wanawake wanaohitaji huduma hiyo wanatakiwa wapate bure lakini wanapata kwa shilingi 1,000 ambapo katika maduka ya watu binafsi wanapata huduma hiyo kwa Shilingi 1,500.

Hali hiyo inatokana na serikali kutokuwa na chombo cha kudhibiti bei ya dawa nchini bali ina chombo cha kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa pekee (TFDA) kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya chakula na dawa ya mwaka 2003. na baraza la Famasia ambalo pia hawahusiki kudhibiti bei ya dawa bali kuhakikisha wafamasia na taasisi zinazotoa taaluma ya famasia zinaenenda kwa mujibu wa sheria yao ya mwaka 2011, ambapo bei hizo za dawa ni moja ya vichocheo vya wizi wa dawa.

Kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya afya nanustawi wa jamii ya mwaka 2004, inaeleza kwamba mara baada ya uhuru serikali ilianza kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wote, lakini kufuatia mdororo wa uchumi miaka ya sabini, ongezeko la watu na kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa mapya na kushindwa kuendesha hospitali na vituo vya afya hivyo ikaanzisha mfumo wa uchangiaji.

Utoaji wa huduma za afya kwa watu wote ni wazo lililoasisiwa na katiba ya Shirika la afya duniani ya mwaka 1948 iliyoazimia kwamba huduma bora za afya ni haki ya msingi ya kila mtu na mpango wa afya ni azimio la Alma Ata lililopitishwa mnamo mwaka 1978 na Tanzania ilisaini maazimio hayo.

I’ve had climbing freshly was the time I spent this hibernate in the Octagon in Wyoming, with Kevin and Gabe.